KHLOE KADARSHIAN ASEMA MWAKA 2017 NDIO WA MAFANIKIO YOTE KWAKE... kisa ni ujauzito alioupata mwaka huu

MREMBO  Khloe Kadarshian amesema kwamba katika maisha yake yote mwaka 2017 ndio wenye mafanikio yote.

Staa huyo kutoka kwenye famlia inayorusha kipindi cha "Keeping up with the Kardashians" anatarajia kupata mtoto baada ya kupewa ujauuzito na mpenzi wake Tristan Thompson.

“Kuna mambo mengi yametokea mwaka huu lakini kubwa ni hili la mimi kushika ujauzito na kunifanya nitarajie kiumbe,” alisema staa huyo.


“Nina furaha kutarajia mtoto, haya ni mafanikio makubwa kwangu, huu mwaka umenitendea haki,” aliongeza. 

Khloe Kadarshian amejipatia utajiri kupitia kampuni yake ya mavazi inayojulikana kwa la "Good American."

No comments