KOCHA AMMY NINJE KUONGEZA WATATU KIKOSINI KILIMANJARO STARS

KOCHA wa timu ya Kilimanjaro Stars, Ammy Ninje amepewa nafasi ya kuongeza wachezaji watatu katika kikosi chake ambacho kitashiriki michuano ya kombe la Chalenji.

Shirika la soka Tanzania (TFF) limempa mwanya huo kocha ili kukiongezea nguvu kiweze kufanya vema katika michuano hiyo ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

TFF imempa idhini hiyo baada ya kuona CECAFA imeziruhusu nchi za Uganda na Rwanda kuongeza idadi ya wachezaji watakaoshiriki Chalenji mwaka huu.

Timu za Uganda na Rwanda zinashiriki fainali za ubingwa wa mataifa ya Afrika (CHAN) Januari mwakani ambazo zinahusisha wachezaji wanaocheza Ligi za nchini mwao hivyo CECAFA imewapa nafasi Amavumbi na Uganda kwenda na wachezaji 23.

Ili kuondoa migongano, CECAFA  pia imetoanafasi kwa mataifa mengine kuongeza idadi ya wachezaji wake katika michuano ya Chalenji.


CECAFA Challenge inatarajia kufanyika kuanzia Desemba 3 hadi 16 mwaka huu ambapo wachezaji wote walikuwa kambini kasoro Daniel Lyanga wa Fanja ya Oman ambaye amechelewa kuwasili.

No comments