KOCHA KILI STARS AWATULIZA MASHABIKI MECHI DHIDI YA LIBYA

KUELEKEA mchezo wa Kilimanjaro Stars dhidi ya Libya katika michuano ya Kombe la Chalenji, kocha Ammy Ninje amewatoa hofu Watanzania kwa kuahidi ushindi katika mechi hiyo.

Kilimanjaro Stars imepangwa kuanza dhidi ya timu ya Libya katika mchezo utakaochezwa Desemba 3.

Taifa hilo linasifika kwa umiliki mkubwa wa mchezo na kocha amesema ameshafanyia kazi suala hilo.

“Nikuhakikishie, siku ya kwanza tu nilipopata nafasi ya kufundisha Kilimanjaro Stars nilianza kuangalia mikanda ya video ya Libya katika michuano ya Chalenji kwani naufahamu ubora wao na udhaifu vizuri tu sina mashaka na hilo,” alisema kocha huyo.

“Niwatoe hofu Watanzania, nakiamini kikosi changu, nakijua kikosi nilichonacho, tunakwenda kushinda,” alisema Ninje

“Nafahamu shauku ya mashabiki katika michuano hii, hatutawaangusha kwani tunakwenda kupambana kwa ajili ya heshima ya taifa letu,” alimalizia.

No comments