KUPAZA, WANINGA WAPIKA MPYA NNE KAMBINI TUNDURU

SALLEH Kupaza baada ya kuunganisha nguvu na mkali wa kucharaza ngoma, Hamza Salleh “Waninga”, wameamua kuweka kambi ya miezi miwili Wilayani Tunduru mkoa Songea wakijiandaa na ujio wa Ivory Band mpya.

Hadi hivi sasa Ivory Band iliyoungana na W Music Band ya Waning, tayari imeshapika vibao vinne moto wa kuoteambali, ambavyo baadhi yake ni “Singeli ya Kisasa” kilichotungwa na Waninga pamoja na “Najiamini”, “Baby” ambavyo ni makucha ya Kupaza.


Kwa mujibu wa Waninga, wamepanga kuweka kambi hadi mwanzoni mwa mwezi Februari, 2018 watakaporejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya utambulisho rasmi sambamba na kuanza maonyesho kwenye kumbi mbalimbali. 

No comments