LIVERPOOL YAFANYA 'KUFURU' CHAMPIONS LEAGUE ... yaifumua Spartak Moscow 7-0, Coutinho apiga hat-trick


Coutinho doubled the advantage after a sweeping move, finishing into the bottom corner after a Roberto Firmino pass

Liverpool imetinga hatua ya 16 bora ya Champions League kwa kishindo baada ya kuifumua Spartak Moscow 7-0 kwenye mchezo wa upande mmoja wa kundi E.

Mshabuliaji wa Kibrazil Philippe Coutinho alifunga mabao matatu huku Sadio Mane akifunga mara mbili, Roberto Firmino Mohamed Salah kila mmoja akifunga bao moja.

Liverpool imemaliza hatua ya makundi kwa kujikusanyia pointi 12 na kushika nafasi ya kwanza kundi E.


No comments