LUIS ENRIQUE KOCHA MTARAJIWA PSG … Unai Emery kutimuliwa mwishoni mwa msimu


Paris Saint-Germain inadaiwa itamtema kocha wake Unai Emery mwishoni mwa msimu huu huku nafasi yake ikitarajiwa kuchukuliwa na bosi wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique.

Emery, ambaye alitua PSG mwaka 2016 akitokea Sevilla ya Hispania, amekuwa na mwendo mzuri kwenye Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) lakini bado ameshindwa kuwashawishi waajiri wake juu ya uwezo wake wa kutwaa Champions League.

Kitendo cha kufungwa 2-1 kwenye League 1 na timu iliyopanda daraja, Strasbourg na baadae kulambwa 3-1 na Beyern Munich katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa, kimemchefua rais wa timu Nasser Al-Khelaifi na sasa anaamini Emery si mtu sahihi katika kusaka mafanikio ya Ulaya.

Mbali na Luis Enrique, makocha wengine wanaohusishwa na PSG ni Massimiliano Allegri, Antonio Conte, Diego Simeone na Jose Mourinho.


No comments