Habari

LWANDAMINA AILIA “CHABO” SHELISHELI KUELEKEA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA

on

PAMOJA na uwepo wa ratiba za
michuano ya Kombe la FA, Kombe la mapinduzi na Ligi Kuu bara, kocha wa Yanga,
George Lwandamina ameanza kuifuatilia klabu ya St. Lois ya Shelisheli ambayo
watakumbana nayo katika mzunguuko wa kwanza Klabu Bingwa Afrika.
Lwandamina amesema kwamba klabu
ya St Lois imefanya mabadiliko makubwa ya kiufundi na hawataingia uwanjani kwa
kuidharau hata kidogo.
“Nimetumia muda mwingi
kuifuatilia, sio timu nyepesi kama ambavyo watu wanazungumza hivyo tunalazimika
kuingia uwanjani kwa kutoidharau kama tunataka kusogea mbele,” alisema
Lwandamina.
“Wamewekeza vizuri katika
kikosi chao, hatutawadharau hata kidogo, kuna mapinduzi makubwa kwenye soka
katika miaka ya hivi karibuni, hakuna timu ndogo wala kubwa. Ukizembea timu
yoyote itakuadhibu,” aliongeza.
“Lengo letu ni kuvuka hatua tuliyoishia
msimu uliopita na kwa kuanza lazima tuonyeshe hilo kuanzia mechi ya kwanza bila
kujali tunakutana na timu kutoka ukanda upi.”
Katika droo iliyofanyika makao
makuu ya Shirikisho la soka Afrika (CAF), timu 59 zimepangwa katika Ligi ya
mabingwa na 44 zimo katika Kombe la Shirikisho.

Yanga ikivuka hatua hii
itakutana na mshindi kati ya Township Rollers ya Botswana na El Merreikh ya
Sudan.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *