MAJERUHI THABANI KAMUSOKO KUPELEKWA INDIA KWA MATIBABU ZAIDI

YANGA inataka kumaliza tatizo ya kiungo wake Thabani Kamusoko na sasa yuko mbiooni kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.

Taarifa kutoka ndani ya kamati ya mashindano ni kwamba Kamusoko ambaye amekosa mechi nyingi kwa kuwa majeruhi sasa mabosi wa klabu hiyo wanapanga kulimaliza hilo haraka.

Bosi huyo wa Yanga amesema amelazimika kuwasiliana na madaktari bingwa wa matatizo ya wachezaji ambapo kiungo huyo atasafiri haraka wiki ijayo kufanyiwa vipimo na kutibiwa kabisa.

Mbali na Kamusoko pia mshambuliaji Amissi Tambwe naye huenda akaunganishwa katika safari hiyo kutibiwa tatizo la goti lake.

‘Tunafikiria kufanya hivyo unajua kamusoko kuumia kweke kumepunguza kasi ya timu yetu sasa tunachotaka ni kumaliza hili haraka,” alisema bosi huyo.


“Tunataka afanyiwe vipimo lakini baada ya kuonekana tatizo atibiwe kabisa ili tujue tumelimaliza hili pia tunafikiria hata Tambwe kama tutaendelea naye akafanyiwe vipimo huko kabisa.”

No comments