MAKOCHA WAWILI WA KIBONGO "WAULA" CHALLENGE CUP MWAKA HUU

MAREFA wawili kutoka Tanzania wamepata nafasi ya kuchezesha michuano ya Kombe la Chalenji nchini Kenya ambayo inatarajia kuanza Desemba 3 hadi 16.

Marefa waliochaguliwa ni pamoja na Heri Sasii na mshika kibendera Soud Lila ambao wameondoka Jumatano hii kuelekea nchini Kenya.

Nafasi nyingine imekwenda kwa Sunday Kayuni ambae ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi pamoja na Mtanzania mwingine, Ahmed Idd Mgoyi.

Michuano ya CECAFA Challenge ilianza mwaka 1926 ikijulikana kama Kombe la Gossage hadi mwaka 1966 ambapo imekuwa ikibadilika jina mara kwa mara.


Timu ya Uganda, The Cranes pia ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kutwaa taji la michuano hiyo mwaka 2015 nchini Ethiopia baada ya kuwafunga Rwanda kwa bao 1-0 mjini Addis Ababa.

No comments