MANCHESTER CITY, SANCHEZ SASA KITAELEWEKA DIRISHA LA JANUARI MWAKANI

KLABU ya Manchester City imepania kuhakikisha inanasa huduma ya mshambuliaji wa timu ya Arsenal, Alexis Sanchez mwenye miaka 28.

Man City walituma ofa mbili kwa Arsenal ambazo zimepigwa chini, lakini sasa wanataka kumalizana nae katika dirisha dogo la Januari.


Staa huyo raia wa Chile anaweza kuondoka bure mwishoni mwa msimu kwani mkataba wake utakuwa umefika tamati kwa klabu hiyo ya jijini London.

No comments