MANYIKA PETER AFUNGUKA KILICHOMWONDOSHA SIMBA SC

KIPA kinda anayetamba katika lango la singida United na timu ya taifa ya Tanzania, Peter manyika Jr amesema kuwa Simba hapakuwa salama kwake na kwamba ndio sababu aliamua kuachana nayo na kwenda kujiunga kwenye kikosi cha Hans Pluijim.

Manyika amesema kuwa kulikuwa na mambo mengi ya kimaisha ambayo yalichangia kuanza kuwekwa benchi katika kikosi cha Simba na kuamua kuitema baada ya mkataba wake kumalizika.

“Kuna vitu viliingiliana kati ya kazi na maisha yangu binafsi, hivyo vitu nadhani vilinigharimu kiasi cha kuanza kuwekwa nje ya kikosi,” alisema kipa huyo.

“Sisi ni vijana na kuna mambo mengi ambayo huwa tunapitia, lakini nashukuru wakati huu nimeweza kukaa sawa kiakili na ndio maana kila kitu kinakwenda sawa,” aliongeza.

“Ni muhimu kujua wapi ulikosea ili iwe rahisi kujipanga upya na kusimama imara kama mwanasoka mwenye ndoto.”

Manyika Jr ameidakia Singida United mechi zote 11 hadi sasa za msimu huu na kuisaidia timu hiyo kupata pointi 20 na kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa ni tofauti ya pointi tatu na vinara wanaoongoza Ligi hiyo.

Katika mechi hizo 11 Singida United imepoteza mchezo mmoja huku ikiwa haijaruhusu kufungwa goli katika mechi saba.

No comments