MAPENZI MUBASHARA KWENYE FILAMU YA WALE OJO YASHUSHA HESHIMA YA MREMBO OMOTOLA JALADE

BAADA ya staa wa Nollywood, Wale Ojo kuibuka na kusema kuwa maeneo ya mapenzi aliyokuwa aliyokuwa akiigiza na mrembo Omotola jalade kwenye filamu yao mpya yalikuwa ni halisi, kumeibuka malumbano mengi kwenye mitandao ya kijamii.

Omotola, mke wa rubani wa ndege, Matthew Ekeinde amesema kuwa alipata kibali kutoka kwa mpenzi wake kabla ya kuanza kuigiza maeneo hayo.

Wale Ojo amesema kwamba hapakuwa na teknolojia yoyote iliyotumika kuhariri maeneo hayo kwani kila kitu kilichofanyika humo kilikuwa ni halisi, jambo lililoanza kushusha heshima ya Omotola.

Mitandao ya kijamii inamshambulia Omotola kutokana na kukubali kupiga picha hizo ambazo ziko nje ya maadili ya Kiafrika.

“Naheshimu sana ndoa yangu na kila kitu kinachohusiana na mapenzi, kwenye filamu yoyote lazima nimshirikishe mume wangu,” amesema Omotola katika taarifa aliyoituma kwenye mitandao ya kijamii.   


Wale ameigiza kama mpenzi wa Omotola Jalade katika filamu hiyo na kuonyeshana mahaba mazito.

No comments