MASHABIKI WAMRUDISHA SELENA GOMEZ KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

MREMBO Selena Gomez ambaye aliamua kuachana na mitandao ya kijamii moja kwa moja baada ya kukerwa na uzushi mwingi, amerudi kwa kasi katika mitandao hiyo.

Selena aliweka msimamo kuwa hatoonekana katika mtandao wa Instagram kwa miaka miwili na kuamua kuishi maisha ya kificho lakini jambo hilo linaonekana kuanza kumshinda.

Mashabiki wa Selena Gomez walikerwa na uamuzi huo, jambo linalotajwa kuwa chanzo cha staa huyo kuamua kujiweka tena hadharani.


Maisha binafsi ya staa huyo na hasa yale yanayohusu mahusiano ya kimapenzi, yametajwa kuwa moja kati ya sababu zilizosababisha awe na idadi kubwa ya wafuasi na kuchochea mauzo ya kazi zake za kimuziki.     

No comments