MOBBY MPAMBALA AWATAKIA MASHABIKI WA BONGOMUVI KHERI YA MWAKA MPYA

MKALI wa Bongomuvi, Mobby Mpambala amewaombea kheri mashabiki na wadau wote wa sanaa ya filamu akisema kuwa anatamani kuona wanafunga na kufungua mwaka wakiwa pamoja tena wenye afya tele.

Akiongea na Saluti5, Mobby amesema kuwa anamuomba Mungu mwaka huu uishe salama na kuuona mwaka mwingine mpya wa 2018 kwa furaha zaidi.

“Namuomba Allah atujaalie waja wake tuuone mwaka mpya tukiwa na furaha na baraka tele, ishaallah," amesema Mobby.

No comments