MRISHO NGASSA AACHANA NA MBEYA CITY NA KUTIMKIA KWA WALIMA KOROSHO

KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Tanzania, Mrisho Ngassa ameachana na Mbeya City baada ya mwaka mmoja kufuatia kumaliza mkataba wake na anaweza kuibukia Ndanda FC ya Mtwara.

Ngassa ni kati ya wachezaji wawili walioondoka Mbeya city wakati dirisha dogo la usajili likifunguliwa na habari zinasema anaweza kuhamishia maisha yake Mtwara.


Ngasa alijiunga na Mbeya City Desema 15, mwaka jana akitokea Fanja SC ya Oman aliyodumu nayo kwa mwezi mmoja na ushei tu.

No comments