MUSSA KIJOTI ASEMA "NINA DENI KUENDELEZA ALIPOACHIA KAKA YANGU"

MUSSA Kijoti ambaye ni mdogo wa aliyekuwa staa wa mipasho katika bendi ya Five Stars Modern Taarab, Issa Kijoti, amesema anafanya jitihada kuhakikisha anaendeleza palea alipoachia kaka yake.

Marehemu Issa Kijoti alipoteza maisha kwenye ajali iliyoua wasanii 13 wa Five Stars usiku wa kuamkia Machi 22, 2011 Mikumi Morogoro wakati wasanii hao wakirejea jijini Dar es Salaam kutoka Mbeya walikokuwa wamekwenda kufanya shoo.

Akiongea na Saluti5, Mussa amesema kuwa anahisi ana deni kuendeleza ustaa wa kaka yake, hivyo jukumu lake kubwa ni kufanya bidii jukwaani na kuwapakulia mashabiki vitu vitakavyowakwangua roho kila wakati.

No comments