OBI MIKEL AKANUSHA KUREJEA LIGI YA ENGLAND

KIUNGO wa Nigeria, John Obi Mikel amekanusha taarifa zinazomuhusisha kutaka kurejea tena katika Ligi Kuu ya England kwenye dirisha la Januari.

Kiungo huyo aliyewahi kuichezea timu ya Chelsea anahusishwa kutaka kurejea kwenye Premier League katika klabu ya Everton.


Obi mwenye miaka 30 amesema kuwa hana furaha kuendelea kucheza soka nchini China katika klabu ya Tianjin Teda.

No comments