OMOTOLA: NAJISIKIA AMANI KUTOJISHUGHULISHA NA MITANDAO YA KIJAMII

MALKIA wa filamu nchini Nigeria, Omotola Jalade amesema kuwa hivi sasa anajisikia huru baada ya kuachana na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Omotola amesema kwamba mwanzo alikuwa na uraibu wa kutupwa na aliona ni vigumu kwake kukaa mbali na mitandao hiyo kabla ya kuchukua hatua ngumu na kuachana nayo moja kwa moja.

“Maisha yangu yalitegemea sana mitandao ya kijamii na hasa blogs, nilikuwa siwezi kumaliza siku bila kuifungua, ni kama ulevi fulani usioachika kirahisi,”alisema Omotola.

“Wakati naamua kuachana nayo nilihisi kama kufa lakini sasa naona niko huru kabisa na wala sijali yanayoendelea kwenye mitanda hiyo,” aliongeza.


Omotola ni mama wa watoto watatu aliozaa na mumewe rubani wa ndege, Captain Ekiende.

No comments