P. DIDDY AONGOZA KWA MKWANJA MREFU DUNIANI 2017

RAPA wa miondoko ya Hiphop, Sean Combs anayejulikana zaidi kwa jina la P. Diddy amekamata nafasi ya kwanza kwa wanamuziki walioingiza fedha nyingi mwaka huu.

Kwa mujibu wa Forbes, rapa huyo amekamata nafasi ya kwanza akiwa hana albumu yoyote kwa kipindi kirefu.

“Diddy ndio mwanamuziki wa kwanza kuingiza fedha nyingi mwaka huu akiwa na pato la dola Mil 130,” ilisomeka sehemu ya ripoti hiyo.

“Fedha hizo zimetokana na ziara yake ya "Bad Boy Family Reunion Tour", mauzo ya kinywaji cha Ciroc Vodka na kampuni yake ya nguo ambayo imeingiza dola mil 70.”

Mtandao wa Forbes, unaeleza kuwa Diddy amekuwa akiteka soko la biashara kutokana na mvuto wake kwenye jamii.

“Mimi ni mtu wa maisha ya wastani lakini mwenye mtazamo mpana kibiashara, nimeanza kujiusisha na biashara yangu nikiwa na miaka 12,” alisema Diddy.

Wakati huo huo mrembo Beyonce amekamata nafasi ya pili baada ya kuingiza mkwanja wa dola mil 100 kwa mwaka huu.

Mapato ya Beyonce kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na ziara yake ya ‘Formation  World Tour’.

No comments