PAPA UPANGA AIBUKIA SEGERE MATATA

MWIMBAJI wa zamani wa Msondo Ngoma Music Band, Papa Upanga ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu tangu ajiengue ndani ya bendi hiyo inayotumia mtindo wa “Baba ya Muziki”, amejiunga na Tabora Jazz Band wana Segere Matata.

Tayari mwimbaji huyo ameifyatulia bendi yake hiyo mpya kibao “Kimya Kingi” ambacho kinaonekana kuwashika vilivyo mashabiki wao katika kumbi mbalimbali wanazotumbuiza.


Wakati akiwa Msondo Ngoma, mwimbaji huyo alitikisa vilivyo kwa kibao chake cha “Machimbo” kinachopatikana kwenye albamu ya “Huna Shukrani”.

No comments