PLUIJIM ATAKA WASHAMBULIAJI WENGINE WAWILI SINGIDA UNITED

KOCHA wa timu ya Singida United Hans Van der Plujim amesema kwamba mpango wake ni kuongeza washambuliaji wawili wazawa katika kikosi chake.

Kikosi cha Plujim hakina tatizo katika safu ya ulinzi kwani kimeruhusu mabao matano tu katika mechi 11 za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Safu ya ushambuliaji haijaonesha matunda baada ya kufunga mabao tisa katika mechi zake 11 za Ligi.

Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba kocha Pluijm anawapa muda zaidi washambuliaji wake wa kigeni Mnyarwanda Danny Usengimana na Mzimbabwe Michelle Katsavairo kabla ya kuwaongezea nguvu.

Festo amesema kuwa wachezaji wengi wa kigeni wanapokuwa katika Ligi mpya ni nadra kuanza na moto, mara nyingi huanza kufanya vizuri katika msimu wa pili, hii ndio sababu ya Pluijm kuendelea kuwavumilia Esengimana na Katsavairo.


Singida United imeachana na wachezaji wazawa, Atupele Green na Pastorya Thanas pia ikiwatoa kwa mkopo wachezaji wake wengine wawili, Mohamed Titi na Frank Zakaria hivyo kocha amepanga kunasa wengine wawili kuongeza nguvu kikosi.

No comments