RAFA BENITEZ AWAPASHA MASHABIKI WA NEWCASTLE: "SITOFUJA PESA USAJILI WA DIRISHA LA JANUARI"

KOCHA wa timu ya Newcastle, Rafael Benitez amesema mashabiki wasitarajie matumizi makubwa ya fedha wakati wa usajili wa dirisha dogo la mwezi Januari.

Mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakimuweka katika presha wakitaka usajili wa dirisha uvute mastaa wakubwa kuja kusaidia timu.


Benitez ameipandisha daraja timu hiyo baada ya kushuka nayo msimu uliopita akiwa amekabidhiwa dakika za lala salama.

No comments