RAMA PENTAGONE AMWOMBEA MAISHA MAREFU ALLY CHOKY

MWIMBAJI mwanaharakati Rama Pentagone leo Jumapili, Desemba 31, 2017 amemtakia kila la kheri mwimbaji mwenzie wa muziki wa dansi, Ally Choky katika maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa.

Katika posti yake aliyoitupia kwenye mitandao ya kijamii, Pentagone aliyewahi kufanya kazi pamoja na Choky katika bendi za Extra Bongo na Twanga Pepeta, amemuomba Mungu amzidishie maisha marefu nguli huyo.

"Hbd my brother Ally Choki mpiganaji mwenzangu Mungu akujalie maisha marefu yenye baraka tuzidi kujifunza mengi kwako igweee Picha ya mapambano," ameandika Pentagone kwenye posti hiyo aliyoiambatanisha na vikatuni vya furaha.

No comments