RAMSEY NOAH AAMUA KUFUNGUKA KUHUSU ASILI YAKE

CHOTARA wa Nollywood, Ramsey Noah kwa mara ya kwanza ameibuka na kutetea uraia wake baada ya kuanza kushambuliwa kutokana na rangi yake.

Ramsey amesema kwamba anapenda kuonekana mnigeria lakini ukweli ni kwamba yeye ni mchanganyiko wa Israel na Lebanoni kwa sababu wazazi wake wana asili hiyo.

“Mimi natumia hati ya kusafiria ya Nigeria lakini ukweli ni kwamba damu yangu ina mchanganyiko wa mataifa mawili; moja ni Lebanoni na linguine ni Israel,” alisema staa huyo.

“Nimezaliwa na kukulia Nigeria lakini wazazi wangu wana asili ya Lebanoni na Israel, hivyo najivunia kuwa hapa,” aliongeza.


Noah amesema kuwa asingependa rangi yake kuwa sehemu ya mjadala katika mitandao ya kijamii kwani ana hisia zote za kuwa raia wa Nigeria kwa sababu amekulia hapo.

No comments