RIHANNA AFICHA PETE YAKE YA UCHUMBA KUKWEPA "MASHILAWADU"

STAA wa muziki nchini Marekani, Rihanna ambaye hivi sasa yupo jijini London na mpenzi wake, Hassan Jameel alificha pete ya uchumba alipokuwa kwenye uwanja wa ndege wa Hearthlow London akikwepa picha za mapaparazi.

Rihanna alificha kiganja chake kwenye koti alilovaa na kuwanyima fursa mapaparazi kuweza kuipiga picha.

Staa huyo ambaye uhusiano wake na Jameel umefikisha miezi sita, alivalishwa pete nchini Hispania katika fukwe za bahari.

Uhusiano wa wawili hao umekuwa ukienda kwa kificho kuhofia waandishi wa habari kuwatibulia.

Kabla ya kunaswa na Bilionea Jameel, Rihanna alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na rapa Chris Brown lakini waliachana mwaka 2009 baada ya kushushiwa kipigo kikali na bwana wake huyo.


Kuachana kwao kulitokana na tamko la mahakama ambapo Chris alitakiwa kukaa mbali na dada huyo.

No comments