SEKUNDE 65 ZA MAAJABU YA LUKAKU NA RASHFORD ZILIVYOZIMA NJOZI ZA CSKA MOSCOW


CSKA Moscow imefungwa 2-1 Manchester United kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa kundi A na kuaga rasmi michuano.

United inatinga hatua ya 16 bora kwa kuongoza kundi A ikifuatiwa na Basel huku CSKA Moscow ikiangukia kwenye Europa League.

CSKA Moscow ilipata bao la kuongoza lililojaa utata katika sekunde ya mwisho ya kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Vitinho.

Hata hivyo kipindi cha pili, United ambayo ilitawala mchezo kwa kiasi kikubwa, ikafanikiwa kufunga mabao mawili ya haraka haraka kupitia kwa Lukaku na Rashford na kufanya uwanja wa Old Trafford uzizime kwa kwa furaha.

Romelu Lukaku alifunga bao la kusawazisha dakika ya 64 akimalizia kiufundi pasi safi ya Paul Pogba huku Rashford akifunga dakika ya 65 kufuatia pasi ya Juan Mata.

Manchester United (5-3-2): Romero 6.5; Valencia 6.5 (Tuanzebe 72, 6), Lindelof 6.5, Smalling 6.5, Blind 6, Shaw 7; Herrera 6 (McTominay 67, 6), Pogba 8, Mata 6; Rashford 7, Lukaku 7.5 (Martial 74, 6)

CSKA Moscow (3-4-3): Akinfeev 6; V Berezutski 6.5, Ignashevich 6, Vasin 6; Fernandes 7, Golovin 6.5, Kuchaev 6, Nababkin 6 (Khosonov 90); Vitinho 6.5 (Zhamaletdinov 82), Chalov 6.5 (Gordyushenko 65, 6), Dzagoev 6.5

No comments