SELE MUHUMBA AITAKATISHA MJENGONI CLASSIC BAND

MCHARAZAJI mahiri wa gitaa la Solo, Selemani Shaibu “Sele Muhumba” ameonekana kukonga vilivyo nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi mkoani Arusha alikohamishia mabegi hivi sasa akiwa anaitumikia bendi ya Mjengoni Classic.

Akiwa na bendi hiyo inayofanya poa kwa sasa kwa mikoa ya kasikazini, Muhumba amekuwa kivutio kikubwa katika shoo wanazofanya, hasa kutokana na ucharazaji wake wa nyuzi ambao unaonekana kuwakuna wengi zaidi.


Mjengoni Classic ni mchanganyiko wa wanamuziki wazawa pamoja na wale kutoka nchi jirani ya Congo DRC ambao wana uwezo mkubwa wa uburudishaji wawapo jukwaani.

No comments