TAMBWE ACHEKELEA KUREJEA DIMBANI YANGA

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amis Tambwe amesema amefurahi kuona anarudi kuanza kuitumikia timu hiyo lakini kikubwa anachotaka kufanya ni kurudisha nguvu ya mabao yake.

Tambwe amesema kuwa alikuwa anasubiri kwa hamu kufika hatua ya kupona majeraha yake ambapo sasa anataka kuona anaanza vyema kwa kufunga mabao muhimu kama kawaida yake.

Tambwe alisema bado ana imani ya kuwa sawa kuweza kuitumikia timu hiyo ambapo ameridhishwa na hatua ya uongozi wa klabu hiyo kumvumilia huku pia akishirikiana nao katika matibabu yake.

Alisema, kutokana na safu yao ya ushambuliaji kukamilika ana imani sasa Yanga itakuwa katika wakati mzuri wa kufunga mabao mengi kama kawaida yao.

“Unajua nilikuwa naumia sana kuona wenzangu wanapambana kwa ajili ya timu lakini mimi nikiwa nje, lakini sasa nashukuru nimepona na nipo sawa kuanza kuitumikia timu,” alisema tambwe.


“Timu yetu iko sawa nawakubali wenzangu wote. Nafikiri sasa ni wakati wa mimi kusaidiana na wenzangu kufunga mabao mengi kama ilivyokuwa huko nyuma na uwezo huo tunao.”

No comments