TAYLOR SWIFT ASEMA MITANDAO YA KIJAMII NDIO SABABU YA KUTAMBA KWA KIBAO CHAKE "I DONT TRUST NOBODY"

MWANADADA Taylor Swift amapata mafanikio makubwa kupitia kibao chake cha “I Don’t Trust Nobody And Nobody Trusts Me”ambacho kimefanya auze nakala za kutosha na kupata ziara nyingi za kimuziki.

Taylor ambaye amekuwa na uhusiano wa kimapenzi unaolega lega amevichana vyombo vya  habari kuwa mauzo yake hayatokani na mchango wa vyombo hivyo bali jiotihada zake binafsi.

Staa huyo amedai kuwa alifanya kila hali kujitangaza kupitia mitandao ya kijamii hivyo haamini kama kuna kazi za ziada ilifanywa na mapaparazi katika kuchochea mauzo ya kazi yake.


“Siwezi kubeza mchango wa vyombo vya habari katika kukuza muziki wangu lakini kwa kiasi kikubwa jitihada zangu na matangazo kupitia mitandao ya kijamii vilichochea mafanikio yangu,” alisema staa huyo.

No comments