THOMAS ULIMWENGU MBNIONI KUREJEA UWANJANI

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu ameifariji klabu yake ya AFC Eskilstuna ya nchini Sweden baada ya kuanza kufanya mazoezi makali.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya TP Mazembe ameanza kufanya mazoezi kwenye ufukwe wa bahari huku pia akiendelea na mazoezi ya gym ili kujiweka sawa kabla ya kuingia uwanjani rasmi.

Thomas Ulimwengu ambaye amekosekana kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa muda mrefu alifanyiwa upasuaji wa goti katika hospitali ya Taasisi ya Sayansi ya Michezo mjini Cape Town, Afrika Kusini.

Maumivu ya goti yamemuweka nje tangu januari, mwaka huu akitokea Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kiasi cha kushindwa kucheza.

Lakini kwa sasa anaweza kurejea uwanjani haraka kabla ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi kwa sababu tatizo lake linaelekea kupona kabisa.

Ulimwengu aliibukia katika Taasisi ya Soka Tanzania (TSA), kabla ya mwaka 2019 kwenda Moro United alikokuwa akicheza kwa mkopo hadi mwaka 2010kisha akachanganya vyema karata zake na kwenda timu ya vijana ya TP Mazembe. 

No comments