TOTTENHAM WAJIPANGA KUIBOMOA WESTHAM... wataka kuwania saini ya kiungo Manuel Lanzini

WABISHI wa jiji la London, Tottenham wameanza kusuka mpango wa kunasa saini ya kiungo wa Westham, Manuel Lanzini mwenye miaka 24.

Hata hivyo, mpango huo unaweza kuwa na milolongo kwani kiungo huyo bado ana mkataba mpaka mwaka 2020.


Spurs wanataka kuboresha kikosi chao wakati huu ambapo wanashiriki katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya huku wakiwa na kibarua cha kusaka ubingwa wa England.

No comments