"UENYEKITI YANGA BADO UNAMSUBIRI YUSUPH MANJI"

MILIONEA wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji ametandikiwa zuria jekundu kuweza kurejea katika timu hiyo kwa kishindo na kukalia kiti cha mwenyekiti kama ilivyokuwa awali kabla ya kuandka barua kuomba kujiuzuru nyadhifa hiyo baada ya kukumbwa na matatizo binafsi.

Katibu mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema kuwa ni suala la utayari wake lakini anakaribishwa kwa mikono miwili kwa sababu bado ni mwanachama wao hai.

“Sioni tatizo kwake kurudi, namkaribisha kwa mikono miwili kwa sababu bado ni mwanachama hai wa Yanga na mchango wake unatambulika na wanachama wote,” alisema Mkwasa.

“Najua anahitaji kupumzika lakini ikiwa anataka kurudi tutampokea, ni suala tu la wanachama wetu kuridhia, taratibu za Yanga ziko wazi,” aliongeza.


Manji aliandika barua ya kuomba kujiudhulu nafasi ya uenyekiti lakini mpaka hivi sasa barua hiyo haijajibiwa na uongozi.

No comments