VIONGOZI WA LIPULI MIKONONI MWA TAKUKURU SAKATA LA ASANTE KWASI KUTUA SIMBA SC

SIMBA imeonekana kuzidi kukalia kuti kavu katika usajili wa beki Asante Kwasi kufuatia vigogo wazito wa serikali ya mkoa wa Iringa kukomaa kutaka beki huyo asalie katika klabu hiyo ya Lipuli.

Samba ilikuwa tayari imeshamsainisha Kwasi ili awe beki wao lakini mpango huo umeingia mwiba kufuatia raia huyo wa Rwanda kuwa ndani ya mkataba wa miezi minne.

Taarifa kutoka ndani ya Lipuli zimesema usajili wa Kwasi kutua Simba bado uko katika utata mkubwa ambapo wekundu hao wasipojipanga wanaweza kujikuta wakiingia katika kuvuna adhabu kubwa ya kukiuka usajili.

Bosi huyo alisema tayari vigogo wa Lipuli wameshapokea angalizo kubwa kutoka serikali ya mkoa wao, hasa mkuu wa Wilaya, Richard Kasesera wakitaka kuona viongozi wa klabu hiyo wanataka kufanya hujuma ya kurahisisha usajili huo wa Kwasi kutua Simba wanajulikana haraka.

Tamko hilo limeshaanza kuleta vurugu katika kikosi hicho ambapo tayari viongozi kadhaa wa Lipuli wameshaanza kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), juu ya serikali hiyo.


“Unajua hapa Lipuli sasa kila mtu anaogopa hili suala la Kwasi, unajua serikali ya mkoa ilipambana sana kuhakikisha Lipuli inapanda, sasa hata usajili kuna mambo walichangia na wameshatupa angalizo kwamba wanataka kuona Kwasi anabaki hapa na kuna wenzetu wameshaanza kuhojiwa na TAKUKURU juu ya hili sakata,” alisema mmoja wa viongozi wa Lipuli.

No comments