WES BROWN ASEMA UBINGWA ENGLAND BADO UKO WAZI KWA MAN UNITED HATA KAMA WATAFUNGWA NA MAN CITY


Manchester United na Manchester City zinakutana wikiendi hii katika mchezo utakaochezwa Old Trafford ambao unatarajiwa kutoa taswira ya mbio za kusaka taji baina ya timu hizo mbili zilizoko kileleni.

City inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi nane na iwapo itafanikiwa kuinyuka Manchester United, basi itajitanua kwa pointi 11 safi.

Ikiwa tayari michezo 15 imechezwa na kila timu, beki wa zamani wa Manchester United, Wes Brown anasema ubingwa bado uko wazi hata kama timu yake hiyo ya zamani itapoteza pointi tatu kwenye mchezo huo.

"Hata kama United itafungwa, kamwe sitasema mbio za ubingwa zimefikia tamati," WesBrown aliiambia 888sport lakini akakiri kuwa City itajiweka pazuri iwapo itavuna pointi tatu Old Trafford.


No comments