YANGA KUINGIA KAMBINI JUMATATU KWA AJILI YA MAPINDUZI CUP

KIKOSI cha wachezaji wa timu ya Yanga kipo mapumzikoni wakati huu baada ya kucheza mechi 11 za Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini kocha anahitaji kambi kuanza Jumatatu ijayo.

Lwandamina anaona ni vyema kuanza maandalizi mapema kwa wachezaji waliobaki baada ya kuiongoza Yanga kukamata nafasi ya 3 nyuma ya timu za Simba na Azam zilizoshindwa kuongeza pengo la pointi baada ya kutoka sare katika mechi zao.

Yanga imekwenda mapumziko ikiwa na kumbukumbu ya kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.

Lwandamina ameitaka kambi hiyo mapema kwasababu ya ratiba ya michuano kuwa mingi ambapo katika Kombe la Mapinduzi watacheza dhidi ya JKU ya Zanzibar Januari 1 lakini wakati huohuo wanajipanga na michuano ya klabu Bingwa Afrika.

Wapinzani wao wakubwa Simba wao wameingia kambini jana Ijumaa huku wakiwa kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufungwa baada ya kulingana pointi na watetezi wa Kombe la Mapunduzi, Azam FC.


Ligi Kuu imesimama kwa wiki mbili hadi tatu kupisha michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge.

No comments