YANGA SC YAIKATILI SINGIDA UNITED KWA KIUNGO ALLY NG'AZI

YANGA imeifanyia umafia Singida United kwa kuipokonya kiungo wa maana ambaye inasemekana kuwa alikuwa anatua huko na kugeuza dili kutua Jangwani.

Singida ilikuwa katika hatua za mwisho kumsajili kiungo kinda Ally Ng’anzi aliyekuwa katika kikosi cha Serengeti kilichoshiriki fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwaka huu nchini Gabon.

Baada ya kupata taarifa hizo Yanga inadaiwa walimvamia mchezaji huyo na kumalizana na wakala wake haraka.

Aliyetoa mchoro huo ni mshambuliaji kinda Yohana Mkomola ambaye aliwaambia Yanga mwenzake huyo kwamba iwapo atakwenda Singida watakuwa wamelamba dume.

Ally alifanikiwa kuwa tishio nchini Gabon akicheza mechi zote kwa kiwango bora hatua ambayo mabosi wa Yanga waliapa kufa naye.


Kukamilika kwa usajili huo kutaipa Yanga kufikisha idadi ya wachezaji wanne kutoka katika kikosi hicho cha Serengeti wakiwemo Ramadhan Kabwili, Said Mussa, Mkomola na Ng’anzi.

No comments