YONDAN ASEMA HATISHWI NA UJIO WA BEKI FISTON KAYEMBE YANGA SC

BEKI wa Yanga, Kelvin Yondani amesema hatishwi kwa chochote na usajili wa mlinzi mpya, Fistoni Kayembe raia wa Congo.

Yondani amesema anauamini uwezo wake akiwa uwanjani hivyo hawezi kuwa na hofu yoyote juu ya raia huyo wa Congo, Kayembe.

“Mabeki wengi wamekuja na kuondoka Yanga na hakuna yeyote aliyeniondoa katika kikosi cha kwanza, siri kubwa kwangu ni kuheshimu mazoezi na kufuata miiko ya uchezaji,” alisema Yondani.

Fiston “Festo” Kayembe Kanku ambaye ameletwa na Mkongo mwenzake, Papy Tshishimbi hapa nchini alikuwa kwenye majaribio katika timu ya Yanga kwa muda mrefu na amefanikiwa kulishawishi bechi la ufundi kwa muda aliokuwa kwenye majaribio hivyo kupata mkataba wa miaka miwili.


Ujio wa Kayembe unaifanya safu ya ulinzi ya Yanga kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na kuwa na nyota wengi wenye uwezo mkubwa kama Cannavaro, Yondani, Andrew Vicent, Ninja na Mkongo huyo.

No comments