ZANZIBAR HEROES KUANZA NA RWANDA CHALLENGE CUP LEO

KIKOSI cha timu ya Zanzibar Heroes leo Jumanne kinatupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya Chalenji kitakapoivaa Rwanda kwenye michuano hiyo inayoendelea nchini Kenya.

Michuano hiyo huandaliwa na Shirikisho la vyama vya soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, CECAFA na ilianza Jumapili wakati wenyeji Kenya walipocheza na Rwanda, huku Kilimanjaro Stars ikiivaa Libya.

Zanzibar ipo Kundi moja la A na ndugu zao Tanzania Bara "Kilimanjaro Stars" ambao wao walifungua dimba Jumapili walipowavaa waarabu Libya ambao ni timu mwalikwa kwenye michuano hiyo.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Hemad Suleiman maarufu kama Moroco, kinatarajiwa kutoa upinzani mkali kwenye mchezo huo dhidi ya Rwanda kama ilivyonukuliwa na kocha huyo.

Zanzibar Heroes katika kikosi chake ina wachezaji watatu wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ambao ni mabeki, Abdallah Haji "Ninja" na Haji Mwinyi Ngwali.

Kikosi kamili cha Zanzibar Heroes ni chenye wachezaji 24 ni pamoja na Magolikipa Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang’ombe), Nassor Mrisho (Okapi) na Mohammed Abdulrahman (JKU) walinzi Abdallah Haji Ninja (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed (Jang’ombe),  Adeyum Saleh (Kagera Sugar) Haji Mwinyi Ngwali (Yanga) Issa Haidar (JKU) Abdulla Kheir (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang’ombe).

Viungo Abdul-swamad Kasim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang’ombe) Mudathir Yahya (Singida United) Mohd Issa (Mtibwa Sugar) Amour Suleiman (JKU) na Hamad Mshamata (Chuoni).


Washambuliaji Suleiman Kassim (Majimaji) Kassim Suleiman (Prisons), Feisal Salum (JKU) Khamis Mussa (Jang’ombe Boys) Mwalimu Mohd (Jamhuri) Seif Abdallah (Lipuli) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).

No comments