ABBU OMAR AIPIGA JEKI RUPONDA SEC NACHINGWEA… amwaga kompyuta 10 na kuahidi makubwa zaidi

MWANAMUZIKI mkongwe anayeishi na kufanya shughuli zake za muziki nchini Japan, Abbu Omar “Profesa”, ametoa seti kumi za kompyuta zenye thamani ya shilingi laki nne kila moja, kwa shule ya sekondari Ruponda, Nachingwea, katika harakati za kusapoti mapinduzi ya elimu nchini.

Akiongea na Saluti5, Abbu amesema kuwa ameguswa kutoa kompyuta hizo kutokana na kwamba anafahamu umuhimu wa elimu duniani na ameahidi kujitoa zaidi kila pale atakapojaaliwa kufanya hivyo kiuwezo.

“Unaweza kufikiri labda Abbu najipanga kujiingiza kwenye siasa maana wanasiasa wengi huanza namna hii, lakini kwangu si hivyo. Nimeamua tu kujitolea kusaidia jamii kutokana na kwamba huku ndiko machimbuko yetu yaliko,” amesema mwanamuziki huyo.

“Nawapenda sana hawa watoto wazuri kutoka kijijini kwetu Ruponda -Nachingwea. Bado nina project maalum ya kuwasaidia zaidi kwa mambo mengi watoto hawa na wengine ambao jumla yao ni 120 kutoka katika vijiji vitatu jirani,” amesema.


“This is my big project aiming to help these kids with others, a total of 120 kids from three different villages. May God bless my plans with these beautiful African kids,” aliongeza akimaanisha kuwa mpango wake huo ni mkubwa na umelenga kuwasaidia watoto hao kutoka vijiji vitatu tofauti huku akiomba Mungu amsaidie kufanikisha.

No comments