ABDALLAH HEMBA WA SIKINDE ASEMA HANA PAPARA KWENYE UTUNZI LAKINI...

MMOJA wa waimbaji tegemeo wa Mlimani Park Sikinde, Abdallah Hemba amesema kwamba humchukua muda mrefu kutoka kuachia wimbo hadi kutunga mwingine lakini kila anapofyatua vibao vyake huwa moto wa kuoteambali.

Akiongea na Saluti5, Hemba amesema kwamba utunzi wa mara kwa mara wakati mwingine ndio unaochangia kushusha viwango vya wanamuziki wetu kutokana na kufilisika haraka kwa mawazo ujumbe vichwani mwao.


“Hivi sasa najipanga kuja na wimbo ambao naamini utakuwa habari ya mjini baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu sana,” amesema Hemba ambaye ni miongoni mwa waimbaji vijana hodari wa kucheza na sauti zote.

No comments