ARSENAL NYEPESI HADI HURUMA, YACHAPWA 2-1 NA BOURNEMOUTH


Bournemouth imetumia dakika nne tu kutoka nyuma na kuiadhibu Arsenal katika mchezo wa Ligu Kuu ya England.

Magoli kutoka kwa Callum Wilson na Jordon Ibe dakika ya 70 na 74 yakawapa wenyeji pointi tatu muhumu na kuiacha Arsenal kwenye mazingira magumu.

Hector Bellerin aliipa Arsenal bao la kuongoza dakika ya 52 kufuatia shambulizi la kushtukiza, lakini matokeo ya mchezo huu yanafanya safari ya Arsenal kumaliza kwenye 'top four' iwe ngumu.
No comments