ARSENAL YATOLEWA FA CUP, YACHAPWA 4-2 NA TIMU YA DARAJA LA KWANZA


Arsenal imekula kichapo kitakatifu cha bao 4-2 kutoka kwa timu ya daraja la kwanza, Nottingham Forest kwenye mchezo mkali wa FA Cup.

Kichapo hicho kinahitimisha safari ya Arsenal kwenye mbio za kusaka kombe hilo la pili kwa ukubwa England.

Nottingham Forest ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Eric Lichaj dakika ya 20 lakini Arsenal wakachomoa dakika tatu baadae kwa bao la beki Per Mertesacker.

Kwa mara nyingine tena Eric Lichaj akaifungia Nottingham Forest dakika ya 40 kabla Ben Brereton hajafunga bao la tatu kwa penalti dakika ya 64.

Danny Welbeck akafufua matumaini ya Arsenal kwa kufunga bao la pili dakika ya 79, lakini Kieran Dowell akashindilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao la nne dakika ya 85 kwa mkwaju wa penalti.

No comments