ASHA BARAKA ASEMA NYIMBO NDEFU KAMA RELI YA KIGOMA HAZINA NAFASI TENA TWANGA PEPETA


Bosi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka amesema nyimbo ndefu kama reli ya kwenda kwao Kigoma hazina nafasi tena ndani ya bendi yake.

Akiongea na kipindi cha Weekend Bonanza cha Clouds FM Jumamosi usiku, Asha Baraka akasema wanamuziki wasiotaka kutii agizo hilo basi nyimbo zao zitaozea studio.

“Kuna wanamuziki sugu ndani ya Twanga Pepeta, wanajiona wana majina makubwa na hawataki kusikiliza ushauri, bado wako na mfumo wa kutengeneza nyimbo ndefu na zile ambazo haziendani na soko la sasa, hizi hazina nafasi kwangu,” alisema Asha Baraka na kufafanua kuwa wanamuziki hao ndiyo wamechangia kukwama kwa zoezi la bendi hiyo kutoa albam kila mwaka.

“Mimi nakutana na wafanyabiashara wenzangu tunabadilishana ushari juu ya mwelekeo wa muziki, nakutana na watangazaji wa radio na televisheni wananipa ushauri juu ya nini kifanyike, lakini unapokipeleka kwa wanamuziki wanakuwa wabishi.

“Yale mambo ya kutengeneza nyimbo ndefu kama treni ya kwenda kwetu Kigoma hayapo tena kwenye soko la sasa hivi.

“Kuna wanamuziki wengi wameenda kutengeneza nyimbo studio lakini kila wakizeleta kwangu nazikataa, wakitaka wakazitumie wanakotaka lakini sio Twanga Pepeta,” alifunguka Asha Baraka katika mahojiano yake na Khamis Dacota wa Clouds FM.
-->

No comments