ATHUMAN KAMBI WA MSONDO NGOMA SASA AJA NA KITU CHA "BOSI HANUNIWI"

BAADA ya kuachia kibao “Heshima Iko Wapi”, mwimbaji mahiri wa Msondo Ngoma Music Band, Athuman Kambi amesema yuko mbioni kuibuka na kete nyingine inayokwenda kwa jina la “Bosi Hanuniwi”.

Akiongea na Saluti5, Kambi amesema kuwa anaamini kibao hicho kipya kitakuwa funika kutokana na namna anavyokiandaa kwa utulivu huku akijiribu kukusanya matukio anayoyafahamu kwa kadiri ya uzoefu wake kimaisha.

“Niko namalizia kuandika mashairi ambapo muda si mrefu nitayawakilisha mazoezini ili tuanze kuyafanyia kazi. Nawaomba mashabiki wategemee kitu ambacho ni saizi yao kabisa,” amesema Kambi.

No comments