AUDIO: PATA KIBAO "MPENZI ZARINA" CHENYE HISTORIA NDEFU KWA HASSAN BITCHUKA


WIMBO “Mpenzi Zarina” wa Msondo Ngoma ambao umerekodiwa mwaka 1978 unaweza kuwa na historia ndefu kwa mtunzi Hassan Bitchuka, hasa kwavile alimtungia mkewe aliyenaye hadi sasa wakiwa wamezaa na kujukuu huku pia mwenyewe akisisitiza kuwa ndio tungo bora zaidi kwa upande wake.

Ala za upepo zilizopulizwa kiufundi zaidi na Joseph Lusungu, Betto Julius na Zito Mbunda ndio zinaouanzisha wimbo huu ambao waimbaji wake ni Muhiddin Gurumo, Juma Akida, Lusungu na mwenyewe, Bitchuka.

Katika tungo hii Bitchuka anmevaa uhusika wa mwanaume aliyetorokwa na mpenziwe waliyeishi nae kwa muda mrefu na kuachwa kwenye dimbwi zito la wasiwasi kutokana na kumtafuta sana bila mafanikio.


Dokta Said Mabela amesimama imara kwenye gitaa la Solo la wimbo huo huku Rhythm ikiwa imecharazwa na Abdallah Omary na Agay Kauzeni kwenye gitaa zito la Bass, ambapo ngoma ndogo ni ufundi wake Mabruk Halfani na Mohammed Atuf kwenye Tumba.

Na huu ndio wimbo uliobeba albamu hiyo yenye nyimbo nane, nyingine zikiwa ni "Selemani", "Epuka Tabia Mbaya", "Mwana Acha Wizi", "Uzuri si Shani", "Sogea Karibu", "Vijana Tujitokeze",  na "Talaka".

No comments