AUDIO: SIKILIZA FUMBO LA MVUVI HODARI ALIYECHEMKA KWA "KING FISH" SIKINDE


MWAKA 2008 Mlimani Park “Sikinde” walifyatua albamu inayokwenda kwa jina la “Supu Umeitia Nazi” iliyokusanya vibao takriban sita ambavyo baadhi yake vingine ni pamoja na “Njiwa Manga”, “Heshima”, “Fitina” na “Upendo”.

Lakini leo Saluti5 inakupa fursa ya kusikiliza kibao kingine moto wa kuoteambali kilichomo kwenye albamu hiyo, kiitwacho “King Fish” ambacho ni utunzi wake mwimbaji mkongwe Hassan Rehani Bitchuka “Super Stereo”.

Katika wimbo huu, mtunzi amejaribu kuzungumzia namna mvuvi mkubwa sana alivyoshindwa kumvua samaki aina ya King Fish pamoja na uhodari wake  wa kucheza na bahari kwa miaka mingi.

Walioshiriki kukirekodi kibao hicho ni pamoja na waimbaji Abdallah Hemba, Shaaban Dede na Bitchuka mwenyewe, huku kwenye magitaa kukiwa na Mohammed Idd (Solo), Mjusi Shemboza (Rythm) na Tony Karama (Bass).


Juma Choka ndiye aliyezicharaza Drums katika dakika zote 7:40 za wimbo huo usiochusha kuusikiliza, huku Ally Omary Jamwaka akikoleza utamu kupitia Tumba.

No comments