AUDIO: TX MOSHI WILLIAM ALIVYOSEMA "MTANIKUMBUKA" MWAKA 2004


WAPO watu wengi ambao wamewasaidia sana ndugu zao wakati walipokuwa kwenye mstari, lakini baadae upepo ulipokuja kugeuka na kuyumba kiuchumi, wale ndugu waliosaidiwa wakaanza kuwasengenya na kuwasimanga kwa maneno mbalimbali kanakwamba wamesahau fadhila.

Marehemu Tx Moshi William miaka takriban 14 iliyopita akiwa na Msondo Ngoma alifyatua kibao kinachokwenda kwa jina la “Mtanikumbuka”, akavaa uhusika wa mtu aliyewasaidia mno nduguze huko nyuma na sasa mambo yamemchachia.

Pata kibao hicho ambacho kimo kwenye albamu ya “Kaza Moyo” iliyorekodiwa mwaka 2004 na ambacho waimbaji wake ni mwenyewe Tx Moshi, Muhidin Gurumo, Joseph Maina na Othman Momba ambao wote ni marehemu kwa sasa.


Katika ala “Mtanikumbuka” kimeshirikisha Huluka Uvuruge (gitaa la Solo), Zahoro Bangwe (Rythm), Ibrahim Kandaya (Bass), Anold Kang’ombe (Drums), Ally Rashid (Saxophone) na Hamis Mnyupe na Roman Mng’ande kwenye tarumbeta. 

1 comment

Joseph Sawe said...

Nice stuff!!!

Kaka habari, Kama una nyimbo za 'Muungano band'' muziki wa dansi sio Taarabu... Ningeomba utuwekee humu tuburudike.. Naikumbuka ni bendi ya zamani na ikapotea... Kuna jamaa alikuwa anaitwa japo sina uhakikia, aliitwa 'PETY MAKAMBO' Ule wimbo wake ulikuwa poa sana... Thanks.. Wana Arusha