BABA HAJI TENA NDANI YA MUVI MPYA YA “UWANJA WA NYUMBANI”

WANANCHI wameamua kumpa kibaka mzoefu jukumu la kulinda amani mtaani na kuhakikisha mali za watu majumbani zinabaki salama bila kuibiwa, katika hali inayojipambanua kuwa ni kama vile kwenda sambamba na ule usemi maarufu wa “mchawi mpe mwana kulea”.

Hayo yamo kwenye muvi mpya ya Kibongo inayokwenda kwa jina la “Uwanja wa Nyumbani” inayotazamiwa kutupwa sokoni wakati wowote mwezi huu huku ikishirikisha wakali kibao wanaofanya poa hivi sasa katika sekta ya filamu Bongo.


Baadhi ya wakali hao watakaoonekana katika picha hilo linaloandaliwa na kampuni ya Joh Film, ni pamoja na yule nguli mwenye hisia kali za mapenzi, Haji Adam “Baba Haji”, Said Kiunda, Idd Tukutu, King Sapeto, Salma Said. 

No comments