Habari

CHEKO LIMEREJEA USONI KWA MOURINHO HUKO DUBAI …Valencia na Carrick wampa raha

on

Baada ya kuwa kwenye ‘mchuno’ mkali ile mbaya katika siku za hivi karibuni, hatimaye uso wa Jose Mourinho umeanza kupambwa tena na furaha.
Mourinho ameonekana ni mwingi wa furaha katika kambi yao ya siku chache huko Dubai hususan baada ya kiungo mkongwe Michael Carrick kurejea mazoezini baada ya kuwa nje ya dimba kwa muda mrefu kufuatia tishio la kuweko tatizo kwenye moyo wake.
Mwingine aliyeongeza furaha ya Mourinho ni beki Antonio Valencia ambaye nae amepona na kurejea mazoezini.
Katika siku za karibuni Mourinho amekuwa hana furaha ikichangiwa na vita vyake na wachambuzi wa soka, shutuma za usajili kwa viongozi wa Manchester United pamoja na vijembe vikali dhidi yake na kocha wa Chelsea Antonio Conte.
Antonio Valencia is also back in training after being sidelined through a hamstring injuryAntonio Valencia akiwa mazoezini huko Dubai
 Carrick naye akiwa mazoezini huko Dubai
Cheko limerejea usoni kwa Mourinho

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *