CONTE ASEMA HANA BAHATI YA KUPEWA WACHEZAJI ANAOWATAKA ...awasilisha mapendekezo yake ya usajili


Antonio Conte ameweka wazi kuwa anataka kufanya usajili katika dirisha hili la Januari na tayari ameshaikabidhi bodi ya Chelsea orodha ya wachezaji anaowahitaji.

Miongoni mwa wachezaji wanaodhaniwa kuwemo kwenye list ya Conte ni pamaja na beki wa kulia wa Juventus Alex Sandro na kiungo wa Bayern Munich Arturo Vidal.

Hata hivyo kocha huyo amesema amekuwa na bahati mbaya ya kutopewa wachezaji anaowahitaji.

Kocha huyo wa zamani wa Juventus, ameiambia Sky Sport Italia: "Siweki matarajio makubwa sana juu ya maombi yangu na ukiangalia historia yangu utabaini kuwa mara chache sana ndiyo  nilifanikiwa kupewa wachezaji niliowahitaji".

No comments